King sports world wide.

Breaking News
recent

Simba yaishindilia Ruvu Shooting Mabao 7, Wachezaji walalama

 

Simba wameibuka na ushindi huo dhidi ya Ruvu Shooting na kutinga hatua ya robo fainali na kuungana na Azam FC, Coastal Union, Kagera Sugar, Geita Gold,Yanga, Polisi Tanzania na Pamba.

Mabao hayo yanamfanya Chama kuungana na kina Abdul Suleiman ‘Sopu”, Kinda wa Tunduru Korosho wameingia kambani mara nne, Reliants Lusajo wa Namungo, Eliya Chibula Tunduru Korosho,  Meshack Abraham Kagera Sugar, Paul Peter Azam FC.
 
Wengine waliofunga mabao hayo 'Hati-triki' ni Idd Kipagwile wa KMC alipocheka na nyavu mara tatu wakati timu yake ikiiadhibu Majimaji mabao 4-1, huku Boban Zirintunsya naye akitupia matatu, Mtibwa Sugar ilipoilaza Tunduma United mabao 7-1.

Kama haitoshi naye staa wa Yanga, Heritier Makambo hakuwa mbali kuingia kwenye orodha ya wakali wa 'Hati-triki' alipoiongoza timu yake kutupia mabao 4-0 dhidi ya Ihefu huku yeye akiingia wavuni  mara tatu na Fiston Mayele akihitimisha karamu ya mabao hayo.

Katika mchezo wa Simba uliopigwa uwanja wa Mkapa, mbali na Chama kuingia kambani mara tatu mabao mengine yalifungwa na John Bocco (2), Jimmyson Mwanuke moja na Michael Masinda ambaye alijifunga.

ARCH-FORUM TZ

ARCH-FORUM TZ

No comments:

Post a Comment

Google ads

Powered by Blogger.